Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-SIASA

Kanisa Katoliki DRC lawataka raia kutetea haki zao

Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametoa wito kwa wananchi kuendelea kupigania haki zao na kutokukubali mbinu zozote za Serikali kutaka kuharibu demokrasia ya nchi hiyo.

Kiongozi Mkuu wa Cenco, Askofu Marcel Utembi, na Katibu Mkuu wa Cenco Donatien Nsholé tarehe 30 Desemba 2016, Kinshasa, DRC.
Kiongozi Mkuu wa Cenco, Askofu Marcel Utembi, na Katibu Mkuu wa Cenco Donatien Nsholé tarehe 30 Desemba 2016, Kinshasa, DRC. AFP/JUNIOR D.KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Tangu kutokea kwa makabiliano kati ya polisi na waumini wa kanisa Katoliki juma moja lililopita ambapo watu zaidi ya 6 wameripotiwa kupoteza maisha kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, kanisa hilo halijawa na uhusiano mzuri tena na Serikali ya rais Joseph Kabila.

Akizungumza jana jijini Kinshasa, Padri Donatien Nshole msemaji wa Baraza la maaskofu nchini humo, SENCO, amewataka viongozi kuheshimu haki ya kuandamana kama inavyoelekezwa na katiba.

Hivi leo Askofu wa kanisa Katoliki nchini humo, Kadinali Laurent Monsengwo, anatarajiwa kuendesha misa maalumu jijini Kinshasa kuwaombea watu waliopoteza maisha katika maandamano ya juma lililopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.