Pata taarifa kuu
UJERUMANI-SIASA

Angela Merkel : Tumefikia makubaliano ya kuunda serikali ya muungano

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema chama chake cha CDU kimefikia makubaliano na chama cha upinzani cha SPD, kuunda seriali ya muungano.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (katikati), Horst Seehofer (CSU) na Martin Schulz (SPD), Januari 12 huko Berlin.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (katikati), Horst Seehofer (CSU) na Martin Schulz (SPD), Januari 12 huko Berlin. REUTERS/Hannibal Hanschke
Matangazo ya kibiashara

Kansela Merkel amesema makubaliano hayo, yatasaidia kuunda serikali ya pamoja lakini pia kuleta mwako mpya barani Ulaya.

Mwafaka huu umekuja saa 24 baada ya mazungumzo kati ya vyama hivyo viwili ili kuanza mazungumzo mengine ya kukubaliana namna ya kuunda serikali.

Viongozi wa vyama hivyo viwili walionekana kuwa wachovu na kuwa na macho mekundu baada ya mazungumzo ya usiku kucha, wamewahakikishia raia wa Ujerumani kuwa, serikali hiyo ya muungano itapatikana kufikia tarehe 1 mwezi Aprili.

Mbali na makubaliano ya kuunda serikali ya pamoja, wanasiasa hao wameafikiana kuhusu sera zitazoisaidia kuimarisha Umoja wa Ulaya,lakini pia imekubaliwa kuwa wakimbizi 200,000 ndio wataokakubaliwa kuingia nchini humo kila mwaka.

Suala lingine tata ambalo limeafikiwa ni kuongeza kiwango cha utozwaji kodi.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker amefurahishwa na makubaliano ya wanasiasa nchini Ujerumani na kusema, yatasaidia kuimarisha umoja huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.