Pata taarifa kuu
TUNISIA-MAANDAMANO-USALAMA

Maandamano kupinga mfumuko wa bei yaendelea Tunisia

Maandamano ya ghasia ya kupinga mfumuko wa bei za bidhaa mahitajio yanaendelea kwa siku tatu mfululizo katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na mji mkuu Tunis.

Waandamanaji waendelea kupinga mfumuko wa bei Tunisia.
Waandamanaji waendelea kupinga mfumuko wa bei Tunisia. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Polisi imekua ikijaribu kuzima maandamano hayo kwa kutumia mabomu ya machozi bila mafanikio. Waandamanaji wanaendelea kupinga mfumuko wa bei ambao unaendelea kuathiri upatikanaji wa mahitaji muhimu.

Waziri mkuu , Youssef Chahed ameshtumu waandamanaji akisema kwamba wameendelea kuzua vurugu na wala sio maandamano ya kupinga mfumuko wa bei. Amewatahadharisha wale wote wanaochochea vurugu kupitia maaandamano hayo kwamba sheira itafuata mkondo wake.

Amewataka polisi kutumia uwezo wao ili kuhakikisha kuwa vurugu hizo zinasimama, huku akiwasihi kutovunja haki za binadamu.

Wakati huo huo waandamanaji wameshtumu polisi kujihusisha na vitendo viovu hasa kutumia nguvu zaidi kwa kuzima maandamano hayo, huku baadhi ya waandamanaji wakikamatwa na wengine wakipelekwa sehemu pasipojulikana.

Wafanyabiashara wamekuwa wakikamatwa na polisi na kuibiwa mali zao. Serikali imevitaka vikosi vya usalama kulinda majengo yake kutokana na hasira ya waandamanaji.

Maandamano hayo tayari yamesababisha vifo na watu kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano na polisi katika miji mbalimbali, nchini Tunisia.

Maandamano ni juu ya bei kuwa ghali , wamepandisha, nadhani hii ni hali ngumu sana kubadilika , labda kama rais huyu tutamuondoa"

Kwa mujibu wa chanzo kutoka kwa waandamanaji, siku ya Ijumaa kumeandaliwa maandamano makubwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo, huku polisi ikiimarisha ulinzi katika majengo ya serikali, na barabara kadhaa zimefungwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.