rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Kusini Jacob Zuma

Imechapishwa • Imehaririwa

Jacob Zuma aendelea kukabiliwa na shinikizo la kujiuzulu

media
Kiongozi mpya wa chama cha ANC, Cyril Ramaphosa (kushoto), na Jacob Zuma wakati wa kongamano la chama tawala, Desemba 18, 2017. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC kimefanya mkutano wa faragha hapo jana wakati huu shinikizo zikiongezeka kwa rais Jacob Zuma kutakiwa kujiuzulu nafasi yake kabla ya uchaguzi mkuu wa hapo mwakani.


Hata hivyo taarifa ya chama cha ANC ilieleza kuwa suala la Zuma halikuwemo kwenye ajenda ya kikao hicho ambacho hata hivyo wadadisi wa mambo wanaona kimefanyika kutokana na hofu ya chama hicho kupoteza umaarufu wake kutokana na kashfa za rushwa.

Rais mpya wa chama cha ANC, Cyril Ramaphosa. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Rais mpya wa chama hicho makamu wa rais Cyril Ramaphosa ameahidi kushughulikia changamoto za chama hicho ikiwemo masuala ya rushwa yanayozunguka viongozi wake.

Siku ya Jumatano rais Jacob Zuma, alitangaza Tume kuchunguza madai ya ufisadi serikalini. Hatua hii inakuja baada ya bunge wiki hii kusema kuwa inaanza kuweka mikakati ya kumwondoa madarakani.

Rais Zuma, amekuwa akihusishwa na madai ya ufisadi kuelekea mwaka ujao atapoondoka madarakani.

Kumekuwa na shinikizo hasa kutoka kwa wabunge wa upinzani wakimtajka ajiuzulu lakini pia Mahakama ya katiba, iliipata bunge kosa la kukiuka sheria kuhusu mswada wa kukosa imani na rais Zuma.

Mwezi uliopita mahakama ilimkuta na hatia ya kukiuka hati ya kiapo kwa kukataa kurejesha kiasi cha fedha alichotakiwa kurudisha na kuliagiza bunge kuandaa mchakato utakaotumika kumuondoa madarakani.

Rais Zuma anaendelea kukabiliwa na kashfa ya ufisadi, huku chama cha Nelson Mandela kikiendelea kupoteza wafuasi katika majimbo mbalimbali nchini humo.

Julius Malema mkosoaji na mpinzani mkubwa wa Jacob Zuma amekua akihamasisha wabunge wenzake kuchukua uamuzi wa kumng'atua madarakani Bw Zuma, bila mafanikio.