rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Urusi Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Donald Trump : Kuna uwezekano mdogo mimi kuhojiwa kuhusu Urusi

media
RAis wa Marekani Donald Trump, Desemba 18, 2017. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuna uwezekano mdogo wa yeye kuhojiwa na Robert Mueller, mkuu wa jopo linalochunguza ikiwa timu ya kampeni ya rais Trump ilishirikiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.


Kauli ya rais Trump imekuja baada ya mwanzoni mwa juma hili taarifa kuibuka kuwa mawakili wake wako kwenye mazungumzo na timu ya Mueller kuangalia uwezekano wa yeye kuhojiwa.

Trump amesisitiza kuwa yeye hana cha kuficha na kwamba hii ni kampeni mbaya inayofanywa na chama cha Democrats ambacho amesema baada ya kushindwa vibaya kwenye uchaguzi uliopita, wanatafuta mchawi.

Wakati huo huo Urusi imetupilia mbali ripoti ya baraza la Seneti la Marekani ambayo inaishutumu Kremlin kwa kufanya kampeni na kueneza habari zisizo kuwa na msingi wowote ambazo zinalenga kudhoofisha demokrasia, yanchi hiyo.

Katika Ripoti iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati inayohusika na masuala ya Kidemokrasia na uhusiano wa nje Ben Cardin, ilibainika kuwa Urusi iliingilia Katika uchaguzi wa 2016 Nchini Marekani, kauli ambayo Urusi imekuwa ikikanusha.