Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-UFISADI

Zuma ateua tume ya kuchunguza madai ya ufisadi

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ametangaza Tume kuchunguza madai ya ufisadi serikalini. Hatua hii inakuja baada ya bunge wiki hii kusema kuwa inaanza kuweka mikakati ya kumwondoa madarakani.

Rais wa Afrika Kusini JAcob Zum aanaendelea kukabiliwa na madai ya ufisadi.
Rais wa Afrika Kusini JAcob Zum aanaendelea kukabiliwa na madai ya ufisadi. REUTERS/James Oatway
Matangazo ya kibiashara

Rais Zuma, amekuwa akihusishwa na madai ya ufisadi kuelekea mwaka ujao atapoondoka madarakani.

Kumekuwa na shinikizo hasa kutoka kwa wabunge wa upinzani wakimtajka ajiuzulu lakini pia Mahakama ya katiba, iliipata bunge kosa la kukiuka sheria kuhusu mswada wa kukosa imani na rais Zuma.

Mwezi uliopita mahakama ilimkuta na hatia ya kukiuka hati ya kiapo kwa kukataa kurejesha kiasi cha fedha alichotakiwa kurudisha na kuliagiza bunge kuandaa mchakato utakaotumika kumuondoa madarakani.

Rais Zuma anaendelea kukabiliwa na kashfa ya ufisadi, huku chama cha Nelson Mandela kikiendelea kupoteza wafuasi katika majimbo mbalimbali nchini humo.

Julius Malema mkosoaji na mpinzani mkubwa wa Jacob Zuma amekua akihamasisha wabunge wenzake kuchukua uamuzi wa kumng'atua madarakani Bw Zuma, bila mafanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.