Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-USALAMA

Wanafunzi waendelea kuandamana dhidi ya kupanda kwa bei ya mkate Sudan

Mamia ya wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Khartoum nchini Sudan hapo jana wamekabiliana na polisi wa kutuliza ghasia kwa siku ya tatu mfululizo wakipinga kupanda kwa bei ya mkate.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa kampeni,  Aprili 9 mwaka 2015.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa kampeni, Aprili 9 mwaka 2015. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Toka mwishoni mwa juma polisi wamekuwa wakikabiliana na waandamanaji kwenye miji mbalimbali nchini humo wakipinga kupanda kwa bei ya mkate ambayo imeongezeka mara mbili zaidi katika juma moja baada viwanda kuongeza gharama za uzalishaji.

Maandamano makubwa yalianzia kwenye maeneo yenye vita jimboni Darfur na kwenye jimbo la Blue Nile kabla ya kuenea kwenye jiji kuu la Khartoum ambapo waandamanaji walichoma moto matairi na kufunga njia kabla ya polisi kutumia vitoa machozi kuwatawanya.

Bei ya mkate nchini humo imeongezeka mara mbili zaidi ndani ya juma moja wakati huu ambapo viwanda vya ngano nchini humo vikipandisha bei zao kutokana na Serikali kuzuia uagizwaji wa mbegu kutoka nje.

Polisi wa kutuliza ghasia walikabiliana na wanafunzi wa chuo kikuu cha Khartoum ambapo kwenye mji wa Geneina mwanafunzi mmoja alipoteza maisha wakati wa makabiliano na polisi.

Serikali inasema kwa sasa hali imerejea kuwa shwari kwenye maeneo mengi ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.