Pata taarifa kuu
UINGEREZA-SIASA

Waziri Mkuu wa Uingereza kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ameanza mchakato wa kulibadilisha baraza lake la Mawaziri, baada ya mwaka uliopita kushuhudia serikali yake ikikumbwa na mtikisiko kwa kupoteza umaarufu na kujiuzulu kwa mawaziri wake muhimu kutokana na kashfa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May (Januari 6, 2018) ameanza mchakato wa kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May (Januari 6, 2018) ameanza mchakato wa kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri. Jeff Overs/BBC/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa sasa wa Mambo ya nje, Fedha na masuala ya Brexit hawatarajiwi kuguswa katika mabadiliko haya mpya.

Mabadiliko haya yameanza na Mwenyekiti wa chama tawala cha Conservative, baada ya kujiuzulu kwa kiongozi wa sasa Patrick McLoughlin.

Nafasi yake imechukuliwa na Brandon Lewis, ambaye uteuzi wake umetangazwa kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Wadadisi wa siasa wanasema kuwa, mabadiliko haya ya Baraza la Mawaziri ni kwa Waziri Mkuu Thersa May kuleta mwamko mpya katika serikali yake.

Pamoja na hilo, mchakato wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, pia kutachangia makubwa mabadiliko ya baraza hilo kuelekea mwaka ujao, muda ambao Uingereza intarajiwa kujiondoa kabisa katika Umoja huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.