Pata taarifa kuu
UFARANSA-CHINA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Rais wa Ufaransa azuru China

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hii leo ameanza ziara yake ya kwanza ya kikazi nchini China kwa kutembelea barabara ya Xian yenye historia ya kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na mkewe Brigitte, Jumatatu hii, Januari 8, 2018  Xi'an, katikati mwa China.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na mkewe Brigitte, Jumatatu hii, Januari 8, 2018 Xi'an, katikati mwa China. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Rais Macron atatembelea mji maarufu wa kaskazini mwa China akiambatana na mke wake Brigitte kabla ya kutoa hotuba muhimu itakayohusu mustakabali wa uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Ziara ya siku tatu ya rais Macron ni ishara ya urafiki kati yake na rais wa China Xi Jinping katika mradi wake wa barabara mpya inayounganisha bara Asia na Ulaya kupitia reli, majini na barabara.

Mradi huu unaogharibu kiasi cha dola za Marekani trilioni 1 unalenga kufufua biashara kati ya nchi hiyo na mataifa ya Ulaya na Asia, ambapo ilikuwa inatumika kusafirisha pamba, mazao ya chakula na bidhaa nyingine za thamani.

Nchi ya China imeendelea kusisitiza kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Ulaya na ziara ya Macron ni sehemu ya kuonesha utayari wake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.