rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uchumi Sudani Omar Al Bashir

Imechapishwa • Imehaririwa

Ongezeko la gharama ya mkate lasababisha maandamano Sudan

media
Rais wa Sudan Omar Al Bashir REUTERS/Siphiwe Sibeko

Raia wa Sudan wameendelea kulalamikia ongezeko la bei ya mkate, huku maandamano yakiendelea kushuhudiwa katika miji mbalimbali nchini humo kufuatia kupanda mara dufu kwa gharama ya bidhaa hiyo.


Maandamano hayo yamezuka mara baada ya serikali ya Sudan kuchukua maamuzi ya kuondoa ruzuku ya vyakula na kusababisha gharama ya mkate kupanda mara mbili.

Maamuzi ya kuongeza bei ya mkate kwa serikali ya Sudan ni sehemu ya kufuata matakwa ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) ili kukuza uchumi wa nchi hiyo, ambao umedorora kwa kiasi kikubwa.

Mwanafunzi mmoja aliuwawa na wengine sita kujeruhiwa katika eno la Darfur mara baada ya maandamano hayo kugeuka kuwa ya vurugu.

Serikali ya Sudan pia imezuia magazeti yote yaliyokosoa ongezeko la bei kutouzwa, huku hali ya sintofahamu ikiendelea kushuhudia katika taifa hilo changa la Afrika.

Katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum, waandamanaji waliokua walifunga barabara na kuchoma matairi walisambaratishwa na polisi wakitumia mabomu ya machozi.

Serikali kupitia, Naibu waziri wa mambo ya ndani ilikanusha kuwa maandamano hayo hayakutoea kutokana na ongezeko la bei na kuahidi kuwa atawashughulikia wale wote waliokuwa wanafanya maandamano yenye vurugu.