Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron atoa wito wa ushirikiano kati ya Ulaya na China

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa ziarani nchini China, ametaka Umoja wa Ulaya kujihusisha katika mradi wa kutengeza barabara ya Silk kuunganisha bara Asia na Ulaya, lakini akahimiza kuwa pande zote lazima zigawane faida.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron wanapokea zawadi kutoka kwa mzee mmoja wakati walipotembelea Msikiti mkuu wa Xian katika Jiji la Xian, Mkoa wa Shaanxi, China, Januari 8, 2018.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron wanapokea zawadi kutoka kwa mzee mmoja wakati walipotembelea Msikiti mkuu wa Xian katika Jiji la Xian, Mkoa wa Shaanxi, China, Januari 8, 2018. REUTERS/Ludovic Marin/Pool
Matangazo ya kibiashara

Mradi huo unatarajiwa kugharim Dola Trilioni moja, na barabara hiyo ikikamilika itasaidia kufanikisha biashara kati ya mabara hayo mawili.

Mbali na barabara, Macron amesema bara la Ulaya na Asia, zinastahili kuja na mipango ya kujenga reli ya pamoja katika siku zijazo.

Ufaransa imeendelea kufanya biashara ya China, lakini Biejing imeendelea kuuza zaidi ikilinganishwa na Ufaransa.

Katika ziara yake ya kwanza nchini China, rais Macron amekutana na rais Xi Jinping na kuzungumzia pia umuhimu wa Umoja wa Ulaya kushirikiana na China, kutekeleza mkataba wa mabadiliko ya hewa ili kukabiliana na tabia nchi, licha ya Marekani kujiondoa.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa ziara hii pia itasaidia kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.