Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-CANNABIS-UCHUMI

Australia kuruhusu mauzo ya mihadarati kwa matumizi ya matibabu

Australia imetangaza leo Alhamisi kwamba inakusudia kuwa nchi ya nne ulimwenguni kuruhusu mauzo ya mihadarati aina ya Cannabis kwa nchi za kigeni kwa matumizi ya matibabu, na hivyo kupata sehemu ya soko la wastani la dola bilioni 55.

Australia inatazamia kuanzisha mchakato wa kuuza mihadarati ain aya Cannabis kwa matumizi ya matibabu.
Australia inatazamia kuanzisha mchakato wa kuuza mihadarati ain aya Cannabis kwa matumizi ya matibabu. REUTERS / Andres Stapff
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Kilimo cha Cannabis hakijaruhusiwa kwa watu binafsi nchini Australia na matumizi yake yamepigwa marufuku kwa madhumuni ya burudani. Lakini serikali inatarajia kuwa matumizi ya matibabu, yaliohalalishwa mwaka jana, na maendeleo ya mauzo ya nje yatawwezesha kuongeza kasi ya uzalishaji.

"Lengo letu ni liko wazi: kuwapa wakulima na wazalishaji masharti bora zaidi ili kuwa nchi ya kwanza duniani kuuza nje ya nchi ihadarati kwa matumizi ya matibabu," Waziri wa Afya wa Australia Greg Hunt amewaambia waandishi wa habari katika mji wa Melbourne.

Makampuni katika sekta hiyo, kama Cann Goup, AusCann Group, BOD Australia na Hydroponics Company, zilijikuta kiwango cha fedha kimeongezeka kwa 20% baada ya tangazo hilo.

Idhini ya mauzo ya Cannabis kwa nchi za kigeni itapigiwa kura na Bunge la Australia, na hivyo kuanza kutekelezwa. Bunge linatarajiwa kupiga kura katika kikao cha mwezi Februari mwaka huu. Upinzani kutoka chama cha Labour tayari umetangaza kuwa utaunga mkono hatua hiyo.

Nchi tatu pekee (Uruguay, Canada na Uholanzi) zimehalalisha mauzo ya Cannabis kwa nchi za kigeni. Israeli pia ilitangaza hivi karibuni nia yake ya kufanya hivyo katika miezi ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.