rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Palestina Marekani Israeli

Imechapishwa • Imehaririwa

Palestina: hatutosalimu amri kufuatia vitisho vya Marekani

media
rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, Januri 6, 2016 Bethlehem. REUTERS/Ammar Awad

Palestina inasema haitakubali kutumiwa na Marekani, baada ya kutishwa kunyimwa msaada wa fedha. Marekani imekuwa ikitoa msaada wa kifedha kwa Palestina kusaidia kuimarisha usalama.


Kauli hii ya Palestina imekuja, baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutishia kupunguza, msaada wa kifedha ambao ni Dola za Marekani Milioni 300 kila mwaka.

Wachambuzi wa siasa za eneo la Mashariki ya Kati, wanasema kuwa, tishio hili la Marekani ni kujaribu kuilazimisha Palestina kuja kaatika meza ya mazungumzo na Israel.

Marekani imekuwa ikitoa msaada huo wa kifedha kusaidia kuimarisha usalama lakini pia, kuendeleza maendeleo mbalimbali ya kiuchumi.

Palestina imekuwa ikisema kuwa Marekani kwa kutoa tangazo hilo, haiwezi kuwa msuluhushi asipendelea upande mmoja katika harakati za kutafuta suluhu ya mzozo kati yake na Israel.

Uhusiano kati ya Marekani na Palestina, umekuwa ukiyumbayumba baada ya rais Trump, kutangaza kutambua mji wa Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel.