rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Pakistani

Imechapishwa • Imehaririwa

Marekani yatishia kusitisha misaada yake kwa Pakistan

media
Khurram Dastgir-Khan, Waziri waUlinzi wa Pakistan, alimjibu Donald Trump kwenye Twitter tarehe 1 Januari 2018. Wikimedia Commons/Katarzyna CzerwiƄska

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Marekani itasitisha misaada yake kwa nchi ya Pakistan kwa sababu imeendelea kuidanganya Marekani kwa muda mrefu.


Rais Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa Pakistan inawapa hifadhi magaidi, ambao wanatafutwa na wanajeshi wa Marekani walioko nchini Afghanistan, na kwamba kwa muda mrefu imekuwa ikiwaficha.

Rais wa Marekani pia ameongeza kuwa Pakistan imepokea msaada wa jumla ya dola bilioni Thelathini na nne katika kipindi cha miaka 15 iliyopita na kwamba licha ya makubaliano waliyoafikia hakuna chochote kilichotekelezwa ila uongo na ulaghai, wakifikiria kuwa viongozi wa Marekani hawana akili timamu, amesema Trump.

Marekani inadhamiria kuendelea kuzuia zaidi ya milioni 250 ya msaada kwa Pakistan, ambayo ilichelewesha kwa makusudi kupelekwa kwa taifa hilo la barani Asia, tangu mwezi Agosti mwaka jana.

Wakati huo, Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan, iliahidi kuwa itazidisha juhudi zake za kimataifa za kupambana na magaidi.