rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Iran Hassan Rouhani Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Donald Trump atoa wito kwa mabadiliko nchini Iran

media
Rais wa Marekani Donald Trump aishambulia Iran. REUTERS/Jim Bourg/File Photo

Wakati ambapo maandamano yakiendelea katika mji mkuu wa Iran Tehran na miji mingine nchini Iran, rais wa Marekani Donald Trump amebaini kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba muda wa mabadiliko umewadia nchini Iran. Rais Trump alioneka siku ya Jumatatu akiishambulia Iran.


Wakati huo huo rais wa Iran Hassan Rouhani amemwita Donald Trump adui wa Iran, huku akisema kauli yake haishangazi, kwani anaichukulia Iran kama adui yake mkubwa katika ulimwengu wa sasa.

Kwenye ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, rais Donald Trump amesema “Iran imeshindwa katika nyanja zote, licha ya mkataba uliofikiwa na utawala wa Barack Obama. Wananchi wa Iran wameendelea kuangamizwa kwa miaka mingi. Wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na uhuru. Mali ya Iran inashikiliwa na kundi la watu kadhaa, kama haki za binadamu. Muda umewadia yote hayo kubadilika.”

Katika maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea nchini Iran polisi mmoja aliuawa jana Jumatatu kwa kupigwa risasi.

Taarifa zaidi zinasema zaidi ya watu kumi wameuawa katika vurugu mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza maandamano ya karibuni nchini Iran.

Televisheni ya serikali imesema watu sita waliuawa katika mji wa magharibi wa Tuyserkan baada ya risasi kufyatuliwa.

Kwa upande wake rais Rohanni amesema serikali yake imejipanga kuwashughlikia waandamanaji wanaoipinga serikali hiyo.