rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Urusi Vladimir Putin

Imechapishwa • Imehaririwa

Kiongozi wa upinzani azuiwa kuwania urais Urusi

media
Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny. REUTERS/Maxim Shemetov

Tume ya Uchaguzi nchini Urusi imemzuia Alexei Navalny kuwania urais mwaka ujao. Mwanasiasa huyo wa upinzani alikuwa amewasilsha maombi yake kwa Tume hiyo, baada ya kupata sahihi 500 za uungwaji mkono kutoka katika miji 20.


Tume ya uchaguzi nchini Urusi imesema, Navalny hawezi kuwa mgombea kwa sababu ya mashtaka ya ufisadi, ambayo mwanasiasa huyo ameendelea kuyakanusha na kusema yamechochewa kisiasa ili kuhakikisha kuwa hapambani na rais Vladimir Putin katika Uchaguzi huo.

Mkuu wa tume ya uchaguzi Ella Pamfilova alisema kuwa tume yake inatekeleza sheria ambayo inamzuia Bw. Navalny kushiriki katika kinyang'anyiro cha urais nchini Urusi.

Alexei Navalny, mwenye umri wa miaka 41, amekua kionekana kama mgombea pekee ambaye ana fursa ya kumkabili rais Vladimir Putin.

"Kesi hiyo ilinuia kunizuia kuongea ukweli kuhusu hali ilivyo nchini Urusi, kwa hiyo nitakata rufaa kwenye mahakama ya katiba ya Urusi, " amesema Bw Navalny.

Bw Navalny alipata umaarufu kutokana na kampeni ya kupinga ufisadi na maanadamano dhidi ya rais Putin. Alihukumua kifungo cha nje cha miaka mitano mapema mwaka huu kwa mashtaka yanayohusu matumizi mabaya ya fedha.