Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-ZANU-SIASA

Mkutano mkuu wa chama cha Zanu-PF kufanyika kwa mara ya kwanza baada ya Mugabe

Mkutano wa chama tawala nchi Zimbabwe cha Zanu-PF unafanyika wiki hii nchini humo kuanzia leo Jumanne, Desemba 12 hadi siku ya Ijumaa. Utakua mkutano mkuu wa kwanza wa chama hiki bila kuepo kwa rais wa zamani Robert Mugabe.

Picha ya Emmerson Mnangagwa, rais mpya wa Zimbabwe, ikiwekwa katika ikulu ya Harare
Picha ya Emmerson Mnangagwa, rais mpya wa Zimbabwe, ikiwekwa katika ikulu ya Harare REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Katika tukio hili, rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, anatarajia kuteua makamu wake wawili.

Mkutano huu ulikua fursa kwa Robert Mugabe kumfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa. Lakini hali hiyo ilibadilikakabla ya mkutano huo.

Chini ya mwezi baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyosababisha kujiuzulu kwa Robert Mugabe, Emmerson Mnangagwa anapaswa kuthibitishwa kama kiongozi mkuu wa chama. Na kuteuliwa kama mgombea wa Zanu-PF katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika kabla ya mwezi Agosti 2018.

Hatua ya kufukuzwa kwa Grace Mugabe, mkewe rais wa zamani Robert Mugabe, pia ithibitishwa, pamoja na washirika wake wa karibu kutoka G40, Jonathan Moyo, Saviour Kasukuwere na Makamu wa zamani wa rais Phelekezela Mphoko.

Lakini taadsisi mbalimbali za chama cha Zanu-PF zitarekebishwa. Maveterani au wapiganaji wa vita vya uhuru, waliotengwa kwa miaka kadhaa na Grace Mugabe, wanatazamiwa kuchukua udhibiti wa nafasi muhimu.

Katika tukio hili, rais Emmerson Mnangagwa atawateua Wajumbe Makamu wake wawili. Mmoja kati kati ya watu hao ni Jenerali Constantino Chiwenga, mkuu wa majeshi, alieendesha mapinduzi yaliyosababisha Robert Mugabe kuachia ngazi.

Wiki iliyopita, serikali mpya iliwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka 2018. Bajeti ambayo inaelekea kupata fedha za kigeni ili kuvutia wawekezaji wa kigeni ambao waliikimbia nchi hiyo chini ya utawala wa Robert Mugabe.

Kwa mujibu wa Philippe Van Damme, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Zimbabwe, hatua hizi ni nzuri, lakini hazitoshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.