Pata taarifa kuu
BOLIVIA-SIASA

Morales aruhusiwa kuwania muhula mwingine Bolivia

Mahakama ya Katiba ya Bolivia siku ya Jumanne ilimruhusu rais Evo Morales kuwania muhula mwingine mwaka 2019, ingawa wananchi wa taifa hilo walimkatalia katika kura ya maoni iliyopigwa mnamo mwezi Februari 2016.

Rais wa Bolivia Evo Morales katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu, La Paz Februari 24, 2016.
Rais wa Bolivia Evo Morales katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu, La Paz Februari 24, 2016. REUTERS/Bolivian Presidency/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Evo Morales, mwenye umri wa miaka 58, alishindwa katika jaribio lake la kurekebisha katiba mnamo mwezi Februari 2016 ili kumruhusu kuwania muhula wa nne (2020-2025) baada ya wananchi wa Bolivia kumkatalia katika kura ya maoni ambapo kura ya "Hapana" ilishinda. Chama chake cha MAS kinatafuta kwa njia zote ili kuzuia kura hiyo ya "Hapana".

Katika kutetea uamuzi wake, Mahakama ya Katiba ilmebaini kwamba haki ya kuwania kwa uhuru wadhifa huo ilikuwa kubwa kuliko kikomo kilichowekwa na Katiba.

Kwa mujibu wa Bw Morales, kura ya "hapana" ilipata ushindi mdogo wakati wa kura ya maoni ya mwaka 2016 kwa sababu ya "uongo" uliofichuliwa muda mfupi kabla ya kura.

Kushindwa huko kwa kisiasa kuliwastaajabisha wengi kwa rais wa Bolivia, nchi ya Amerika Kusini, alietawala kwa muda mrefu tangu mwaka 2006.

Evo Morales, anadai kuwa ndiye rais wa kwanza kuongoza Bolivia kwa muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.