Pata taarifa kuu
EQUATORIAL GUINEA-UFARANSA-UFISADI

Mtoto wa rais wa Equatorial Guinea afunguliwa mashitaka

Makamu wa rais wa Equatorial Guinea Teodorin Obiang, ambaye pia ni Mtoto wa rais wa nchi hiyo Teodoro Obiang Nguema, anafunguliwa mashtaka jijini Paris nchini Ufaransa kwa kutumia vibaya fedha za umma akiwa nchini Ufaransa.

Nyumba binafsi ya Teodorin Obiang, katika mtaa wa Foch, nyumba inayopima mita mraba 5,000, ikiwa na vyumba 101.
Nyumba binafsi ya Teodorin Obiang, katika mtaa wa Foch, nyumba inayopima mita mraba 5,000, ikiwa na vyumba 101. AFP/ERIC FEFERBERG
Matangazo ya kibiashara

Teodorin anatuhumiwa kutumia fedha za serikali kununua majengo ya kifahari jijini Paris, na kununua magari ya kifahari.

Mawakili wake wamesema, wanataka kesi hii kuahirishwa ili wapate nafasi ya kutosha kuandaa utetezi dhidi ya mteja wao.

Hii ndio mara ya kwanza kwa Ufaransa kuchunguza kesi dhidi ya matajiri na viongozi kutoka barani Afrika, wanaoishi maisha ya kifahari katika nchi hiyo, huku raia wa nchi yao wakiendelea kuteseka.

Mtoto huyo wa rais Nguema, anatuhumiwa kuwa mfisadi, wizi wa fedha za umma, kuvunja uaminifu na matumizi mabaya ya fedha za wananchi.

Ufaransa ilianza uchunguzi dhidi ya Teodorin mwaka 2011, baada ya kubainika kuwa alikuwa anamiliki nyumba ya kifahari inayokadiriwa kuwa yenye thamani ya Euro Milioni 107.

Mahakama ya Kimataifa ya haki yenye makao yake mjini Hague, ilikataa ombi la serikali ya Equatorial Guinea kuitaka Ufaransa kuachana na kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.