Pata taarifa kuu
ITALIA-SIASA

Gentiloni aunda baraza lake la mawaziri

Jumatatu hii Desemba 12, Paolo Gentilonialikutana na viongozi wa vyama vya siasa kwa minajili ya kuunda serikali ijayo ya Italia na kuhakikisha kwamba ina ungwa mkono kwa dhati na Bunge.

Paolo Gentiloni, Wazuri wa mambo ya Nje wa Italia anaye maliza muda wake.
Paolo Gentiloni, Wazuri wa mambo ya Nje wa Italia anaye maliza muda wake. AFP PHOTO/JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje anayemaliza muda wake alitakiwa Jumapili na rais mpya wa Italia, Sergio Mattarella, kuunda baraza jipya la mawaziri, baraza la 64 katika miaka 70, baada ya kujiuzulu kwa Matteo Renzi, kutokana na kushindwa kwake katika kura ya maoni ya Desemba4 juu ya rasimu ya mageuzi ya kikatiba.

Mwakilishi wa chama cha Democratic Party (cha mrengo wa kati-kushoto, ambapo Renzi na Gentiloni ni wafuasi wa chama hicho) amesema kuwa chama chake kitaunga mkono serikali mpya, huku akisema kufikiria kwamba uchaguzi wa bunge ukokaribu.

Moja ya kazi ya serikali ya Gentiloni itakuwa kuendeleza sheria mpya ya uchaguzi, ambayo kama itapasishwa kwa haraka, inaweza kusababisha kupelekea uchaguzi unafanyika katika awamu ya kwanza katika mwaka 2017.

Italia ina sheria tofauti za uchaguzi kwa Bunge na Baraza la Seneti na rais mpya anasema ni muhimu kuoanisha, ili kuhakikisha kuwa serikali madhubuti inaweza kuibuka katika uchaguzi ujao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.