Pata taarifa kuu
BENKI YA DUNIA-UCHUMI

Jim Yong Kim achaguliwa kwa miaka 5 katika uongozi wa Benki ya Dunia

Mmarekani Jim Yong Kim amechaguliwa kwa mara nyingine tena bila kupingwa kwenye uongozi wa Benki ya Dunia kwa muhula wa pili wa miaka mitano, imesema Jumanne hii taasisi ya maendeleo katika taarifa yake.

Mmarekani Jim Yong Kim, Juni 1, 2016.
Mmarekani Jim Yong Kim, Juni 1, 2016. NICHOLAS KAMM / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano ya kimyakimya yanataka Marekani an Ulaya kugawana uongozi wa taasisi za Bretton Woods. Marekani inashikilia uongozi wa Benki ya Dunia wakati ambapo Ulaya inashikilia uongozi wa Shirika la Fedha Duniani.

Bw Kim, mwenye umri wa miaka 56, alikua kiongozi wa Benki ya Dunia mwezi Julai 2012. Muhula wake wa pili unaanza Julai 1, 2017.

"Wakati nilijiunga na Benki ya Dunia mwaka 2012, kulikuwa na malengo mawili kabambe yaliyohitajika kufikiwa: kumaliza umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 na kukuza mafanikio ya pamoja," Kim amesema katika taarifa yake.

Akitaja changamoto za maendeleo "mabadiliko ya tabia nchi, ukimbizi na magonjwa ya milipuko," ameongeza kuwa Benki ya Dunia inatazamiwa "kufanya kazi zaidi na washirika na kuendelea kutafuta njia za ubunifu kwa ufanisi ili kuinua rasilimali ambazo ni adimu kwa maendeleo. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.