Pata taarifa kuu
BRAZIL-DILMA ROUSSEFF

Baraza la Seneti laamua kumng'atua madarakani Rousseff

Baraza la Seneti nchini Brazil limepiga kura usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano katika neema ya mashtaka dhidi Rais Dilma Rousseff, ambayo ynaweza kusababisha kung'atuliwa kwake mamlakani.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff aliyesimamishwa kwa muda katika majukumu yake, katika Ikulu ya Alvorada, Juni 14, 2016.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff aliyesimamishwa kwa muda katika majukumu yake, katika Ikulu ya Alvorada, Juni 14, 2016. EVARISTO SA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umepitishwa kwa kura 59 dhidi ya 21. Maseneta wamesema kuna ulazima kesi ya kung'atuliwa kwa Dilma Rousseff iwasilishwe ili rais huyo aliyetengwa katika majukumu yake, aweze kuachia ngazi, kutokana na kashfa ya ubadhirifu wa mali ya umma.

Kamati ya Seneti, Alhamisi, Agosti 4, ilipitisha uamuzi kuwa Dilma Rousseff afuatiliwe katika kesi inayomkabili ya utumiaji mbaya wa fedha za umma.

Maseneta walikua wakijadili ripoti kuhusu uchunguzi uliyotolewa mwanzoni mwa wiki hii iliyopita, ambayo ilihitimisha kuwa Dilma Rousseff amepatiakana na hatia, akishutumiwa kutumia fedha za umma ili aweze kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.

Mpinzani wa Dilm aRousseff, aliyekuwa Makamu wa Rais Michel Temer, ataendelea kuwa rais wa mpito. Michel Temer ataongoza aliongoza sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki, bila hata hivyo Dilma Rousseff kuhudhuria sherehe hizo.

Baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili mwaka 2014, rais wa Brazil aliondolewa madarakani na baraza la Seneti Mei 12. Bado anakanusha kuwa hajakiuka Katiba na hivi karibuni alisema kuwa amefanyiwa mapinduzi ya kitaasisi yaliyoandaliwa na vyama vya mrengo wa kulia pamoja na wapinzani wake wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.