Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ANC

Mgawanyiko waendelea kujitokeza katika chama cha ANC

Baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliyopelekea kushindwa kwa sehemu kubwa kwa chama cha ANC, na vyama vya siasa vimeanzisha mazungumzo ili kujaribu kupata mikataba na kuunda muungano katika miji kadhaa mikubwa katika yenye wafuasi wengi wa vyama vinavyounga mkono chama tawala.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, wakati yakitangazwa matokeo ya uchaguzi wa manispaa, ambapo chama madarakani cha ANC kimeshindwa katika miji kadhaa mikubwa.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, wakati yakitangazwa matokeo ya uchaguzi wa manispaa, ambapo chama madarakani cha ANC kimeshindwa katika miji kadhaa mikubwa. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Changamoto ni kubwa mjini Johannesburg na Pretoria na chama cha EFF cha Julius Malema, ambacho kilipata 8% ya kura nchini kote, kinaweza kubadili matokeo. Ila kwa kuwa wakati huu wa mazungumzo unapelekea kuibua mvutano na mgawanyiko ndani ya chama cha ANC.

Jacob Zuma ni moja ya sababu zinazopelkea chaa hiki cha hayati Nelson Mandela Madiola kukumbwa na mgawanyiko. Washirika wengi wa chama hicho wanasita kuunganisha picha zao na ile ya rais ambaye si maarufu.

Chama cha EFF cha Julius Malema ambacho kinachukua nafasi ya tatu katika uchaguzi huo, tayari kimetangaza kuwa kingeliweza kushirikiana na chama cha ANC ikiwa Zuma ataondoka madaraka. Ombi ambalo halikubaliki na wengi.

Mweka hazina wa kundi la vijana kutoka chama cha ANC, amehakikisha kwamba "Zuma hatajiuzulu kwa ajili ya kushirikiana na vyama vingine." Idadi ya makada wa chama cha ANC pia wanakataa wazo la mazungumzo na Julius Malema. Hii itakuwa, kwa mujibu wao, kukubali kwamba mashambulizi yake dhidi ya rais katika Bunge yalikua ya msingi.

Wafuasi wa Jacob Zuma wanatafuta maafisa wengine katika chama hicho: Katibu mkuu wa chama cha ANC Gwede Mantashe, meneja wa kampeni wa chama hicho na hasa serikali za mitaa za mkoa tajiri wa Gauteng.

Maofisa hawa kwa muda mrefu wamekuwa wakikosolewa kwa uongozi mbaya wa chama cha ANC katika ngazi ya taifa na tayari wameamua kushiriki katika majadiliano ya moja kwa moja na Julius Malema, kujaribu kuiokoa miji ya Johannesburg na Pretoria. Lakini itakuwa vigumu kujadili chama hicho kikiwa kimegawanyika.

Julius Malema, kiongozi wa chama cha EFF, Julai 27, 2016 katika mji wa Etwatwa.
Julius Malema, kiongozi wa chama cha EFF, Julai 27, 2016 katika mji wa Etwatwa. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.