Pata taarifa kuu
TAHILAND-KURA YA MAONI

Thailand: upinzani wakabiliwa na shinikizo kabla ya kura ya maoni

Nchini Thailand, wafuasi 19 wa vyama vya kisiasa wameitishwa na polisi na huenda wakazuiliwa jela kwa muda wa mwaka mmoja siku chache kabla kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba iliyoandikwa chini ya uongozi wa serikali ya kijeshi.

Wanaharakati wa Thailandwatoa wito wa kupiga kura ya "Hapana" katika kura ya maoni kuhusu rasimu ya marekebisho ya katiba iliyopendekezwa na serikali ya kijeshi.
Wanaharakati wa Thailandwatoa wito wa kupiga kura ya "Hapana" katika kura ya maoni kuhusu rasimu ya marekebisho ya katiba iliyopendekezwa na serikali ya kijeshi. REUTERS/Chaiwat Subprasom
Matangazo ya kibiashara

Kuitishwa huko ni moja ya ishara ya mwisho ya hali ya wasiwasi ambapo yalifanyika maandalizi ya kura ya maoni itakayofanyika Jumapili Agosti 7. Kupingwa au kukosolewa kwa mswada wa Katiba ni marufuku.

Viongozi wa chama cha upinzani cha Shati Nyekundu (Red Shirts) dhidi ya serikali ya kijeshi, wana tabia ya kukaidi wanajeshi wanaoshikilia madaraka ya uongozi wa nchi. Na wamekua wakitumia muda zaidi katika makao makuu ya polisi ikilinganishwa na muda wanaoutumia katika ofisi za vyama vyao.

Wakati wanaharakati 19 wa kisiasa kati ya viongozi hao walitangaza ufunguzi wa kituo cha kuthibitisha kwamba hakuna udanganyifu katika kura ya maoni ya Jumapili, mara moja waliitishwa kwenye makao makuu ya polisi jirani kwa ukiukaji wa marufuku dhidi ya mkusanyiko wa zaidi ya watu watano.

Maandalizi ya kura ya maoni yalifanyika katika mazingira ambayo hayakua mazuri. Kuwakosoa hadharani rasimu ya katiba ni adhabu ya miaka kumi gerezani. Wasichana wawili wenye umri wa miaka minane wamefikishwa kwenye makao makuu ya polisi kwa kuchana madaftari ya uchaguzi. Wanafunzi ambao walidai kuwepo na udikteta kwa kuandika rasimu ya katiba waliwekwa kizuizini kwa siku kumi na mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.