Pata taarifa kuu
PERU-SIASA

Rais mpya wa Peru achukua hatamu ya uongozi wa nchi

Pedro Pablo Kuczynski, aliyekuwa afisa katika benki ya Wall Street ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Peru mwezi Juni dhidi ya Keiko Fujimori, binti wa rais wa zamani Alberto Fujimori (1990-2000), anatazamiwa kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi Alhamisi hii.

Pedro Pablo Kuczynski akisherehekea ushindi wakeAlhamisi Juni 9, 2016 Lima.
Pedro Pablo Kuczynski akisherehekea ushindi wakeAlhamisi Juni 9, 2016 Lima. REUTERS/Mariana Bazo
Matangazo ya kibiashara

Pedro Pablo kuczynski ana imani ya kuiweka sawa nchi hiyo inayokabiliwa na hali ya sintofahamu katika sekta mbalimbali.

Tangu alipopata ushindi, ambapo aliongoza kwa zaidi ya kura 40,000 tofauti dhidi ya mshindani wake, tayari amesema yuko tayari kunda serikali itakayowahumuisha wanasiasa mbalimbali.

Peru ni moja ya moja ya nchi zinazoendelea kiuchumi katika ukanda wa Amerika ya Kusini kutokana na utajiri wake wa kihistoria wa maliasili (madini), lakini umaskini na kukosekana kwa usawa kumeendelea kuiathiri nchi hiyo.

Uchumi wake umekua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, chini ya utawala wa Ollanta Humala (kutoka mreno wa kushoto), kutoka kwenye kiwango cha ukuaji kwa mwaka cha 6.5% mwaka 2011 hadi 3.3% mwaka jana.

Bw Kuczynski, mwenye umri wa miaka 77, ameahidi kuweka sawa uchumi wa nchi yake, kwa kufufua miradi ya madini, kupunguza umasikini,unaoathiri 22% ya raia wa Peru na kupambana na ukosefu wa usalama katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.

"Changamoto kubwa ni ukosefu wa huduma za msingi kwa 30% hadi 40% ya raia. Hakuna vyuo, usalama kwa wananchi, maji safi au huduma za hospitali. Hizo ni baadhi ya changamoto zinazochelewesha maendeleo, " amesema rais mteule, ambaye ameahidi" mapinduzi ya kijamii ".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.