Pata taarifa kuu
UHISPANIA-UINGEREZA

Waziri Mkuu wa Uhispania aisihi Uingereza

Waziri Mkuu wa Hispania Mariano Rajoy ameionya Uingereza kwamba kama itajiondoa katika Umoja wa ulaya itapoteza haki ya kuishi na kufanya kazi kwa uhuru ndani ya Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, akiambatana na Mkuu wa jiji la London, Sadiq Khan, katika mji mkuu wa Uingereza kwa minajili ya kutetea Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, akiambatana na Mkuu wa jiji la London, Sadiq Khan, katika mji mkuu wa Uingereza kwa minajili ya kutetea Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya. REUTERS/Yui Mok/Pool
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Mariano Rajoy ameyasema hayo katika mahojiano yaliyorushwa Alhamisi hii na shirika la habari la Uhispania la EFE.

Waziri Mkuu wa Uhispania, Mariano Rajoy.
Waziri Mkuu wa Uhispania, Mariano Rajoy. REUTERS/Juan Medina

"Inaonekana kwangu kwamba kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya itakuwa mbaya kwa Uingereza, kwa Uhispania na kwa kwa nchi zote za Ulaya," Bw Rajoy amesema katika video iliyorushwa hewani na shirika la habari la EFE.

"Ulaya iilijengwa kwa msingi ya watu kuwa na uhuru wa kutembea popote wanapotaka barani Ulaya, kuwa na mitaji popote pale na uhuru wa kuingiza bidhaa popote pale, amekumbusha. Kama Uingereza inajiondoa katika Umoja wa Ulaya, wale ambao wataathirika zaidi ni wananchi wa taifa hilo ambao hawatakua na uhuru wa kutembea, au kutuma mitaji na bidhaa. "

"Watulaki moja kutoka Uhispania wanaofanya kazi nchini Uingereza wataathirika zaidi, lakini kuna raia 400,000 kutoka Uingereza wanaofanya kazi nchini Uhispania iambao watajikuta katika hali ya kutisha," Waziri mkuu wa Uhispania asema.

Watu 283,000 kutoka Ungereza wameorodheshwa rasmi kama wanaishi nchini Uhispania lakini idadi halisi inakadiriwa kuwa kati ya 800,000 na milioni moja.

Tarehe 23 Juni raia wa Uingereza watapiga kura ya kubaki au kuondoka katika Ymoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.