Pata taarifa kuu
BRAZIL-SIASA-UCHUMI

Dilma Rousseff awekwa kando na Baraza la Seneti

Alhamisi Mei 12, kwa idadi kubwa ya kura 55 dhidi ya 22, Maseneta wa Brazil wamepiga kura kwa ajili ya ufunguzi wa kesi ya mashtaka dhidi Rais Dilma Rousseff, anayeshtumiwa kutumia kinyume cha sheria mali ya Umma ili kurahisisha kuchaguliwa kwake kwa mara nyingine katika uchaguzi wa mwaka 2014.

Maseneta wa mrengo wa kulia wajipongeza, baada ya kupiga kura ya mwisho ambayo inamuweka kando mamlakani Rais Dilma Rousseff.
Maseneta wa mrengo wa kulia wajipongeza, baada ya kupiga kura ya mwisho ambayo inamuweka kando mamlakani Rais Dilma Rousseff. REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, Rais wa Brazil kwa sasa amesimamishwa mamlakani. Makamu wake wa Rais Michel Temer ndiye atamrejelea kwenye wadhifa huo.

Baraza la Seneti limechukua uamuzi uliochukuliwa mapema na Baraza la Wawakilishi (Bunge), ya kumfungulia Bii Rousseff mashtaka, tukio hili ni la kwanza kutokea nchini Brazil tangu mwaka 1992. Maseneta walikua wakihitajika tu idadi ya Wajumbe 41, lakini uamuzi huo umepitishwa kwa idadi kubwa katika Baraza la Seneti.

Rais atatengwa mamlakani kwa muda wa siku 180. lakini kabla, ifikapo jioni , atalihutubia taifa kwa mara ya mwisho kama Rais. Ni lazima kusisitiza uharamu wa utaratibu, na kuiita bado tena mapinduzi. Inasemekana kwamba atazungumzia akisisitiza kuhusu utaratibu wa kumuweka kando mamlakani ambao haukufuatisha sheria, akiutaja kwa mara nyingine kwamba ni mapinduzi ya kitaasisi. Kisha atajiunga na wafuasi wake wa chama cha PT, na kuandamana kabla ya kuondoka katika Ofisi ya rais na kujielekeza katika Ikulu ya Alvorada, ambapo atakaa kwa kusubiri kesi ya kumng'atua mamlakani moja kwa moja.

Baada ya kesi hii ya Bi Rousseff itafuata kura ya pili ya Baraza la Seneti, kwa theluthi mbili ya kura zinazohitajika (sawa na kura 54), ili kuondolewa mamlakani moja kwa moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.