Pata taarifa kuu
UKRAINE-SIASA-SHERIA

Waziri Mkuu wa Ukraine ajiuzulu

Arseniy Yatsenyuk amekua akikosolewa vikali hasa kwa kuchelewa katika utekelezaji wa mageuzi na kwa sababu alikua akitetea maslahi ya vigogo pekee.

Waziri Mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk katika mji wa Kyiv, Machi 16 2016.
Waziri Mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk katika mji wa Kyiv, Machi 16 2016. REUTERS/Valentyn Ogirenko
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kujiuzulu kwake ambalo limetolewa Jumapili hii linakuja miezi miwili baada ya kuponea Bunge kusita kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Arseny Yatsenyuk anajidai kuwa "kiongozi mkweli wa kitaifa" ambaye anatateta maslahi ya Ukraine. Na kusema kwamba, ndo kinachopelekea anajiuzulu. Waziri Mkuu anaondoka, huku akilaani mgogoro wa kisiasa na kuahidi kuwa ataendelea kutetea maslahi ya Ukraine.

Vikao viwili vya baraza la mawaziri ambavyo Arséni Yatsenyuk alivyoendesha miaka miwili iliyopita vimeiweka nchi hiyo katika hali aya sintofahamu, katika nyanja ya fedhasawa na ile ya kijeshi. Lakini Waziri Mkuu ameshindwa kutekeleza mpango mpana wa mageuzi yanayoendana na kanuni za Umoja wa Ulaya amzo zilitarajiwa baada ya "Mapinduzi ya heshima."

Badala yake, Arseny Yatsenyuk anashukiwa kulinda vigogo wakuu wa nchi hiyo na kufurahia mfumo rushwa ambayo imekua sugu. Kujiuzulu kwake, ambapo kutaidhinishwa Aprili 12, kunamuachia na fasi Volodomyr Groysman, Spika wa sasa wa Bunge na mtu wa karibu wa Rais Petro Poroshenko. Groysman, hata hivo, ameonekana dhaifu kwa wiki kadhaa, kwa sababu anashtumiwa kutumia kuingilia kazi vyombo vya sheria ana dosari kufuatia ufunuo wa kashfa ya ukwepaji kodi kuhusu makampuni yake "Papers Panama".

Kazi alizozifanya Arseny Yatsenyuk

Arseniy Yatsenyuk ni mchapakazi kwa kweli: Aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Uchumi wa Jamhuri inayojietgemea ya Crimea mwaka 2001, kisha Naibu mkurugenzi wa Benki ya Taifa ya Ukraine mwaka 2003, baadaye Waziri wa Uchumi mwaka 2005, Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 2007. Aliongoza maandamano mwaka 2013 dhidi ya Rais Viktor Yanukovych akishtumu rushwa na akateuliwa Waziri Mkuu siku tano baada ya kutimuliwa kwake. Kisha akajikubalisha "kutetea uhuru wa nchi hiyo dhidi ya uvamizi wa jeshi la Urusi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.