Pata taarifa kuu
BENIN-KUAPISHWA-SIASA

Benin: Patrice Talon aahidi kufanya muhula 1 madarakani

Patrice Talon, ambaye ni mfanyabiashara aliyechaguliwa tarehe 20 Machi amepishwa katika uwanja wa mpira wa miguu wa Charles de Gaulle wa Porto Novo.

Patrice Talon akiwasili mjini Cotonou, Benin, Machi 20, 2016.
Patrice Talon akiwasili mjini Cotonou, Benin, Machi 20, 2016. © REUTERS/Charles Placide Tossou
Matangazo ya kibiashara

Mashaka yamemalizika nchini Benin: Kulikua na mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Patrice Talon, Rais mpya na mtangulizi wake Thomas Boni Yayi.

Sherehe zilikua rahisi na zimefanyika katika umakini mkubwa. Rais Patrice Talon aliwasili muda mfupi baada ya saa nne mchana pamoja na mkewe katika uwanja uliokua umefurika umati wa watu.

Rais Talon ameapishwa, huku akipokelewa na Jaji mkuu wa Mahakama ya Katiba kabla ya Spika wa Bunge na Jaji mkuu wa Mahakama kuu.

Mizinga ishirini na mojailifyatuliwa hewani wakati wa sherehe ambayo imehudhuriwa na Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Lionel Zinsou, alieshindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais na ameshangilia na umati wa watu. Wawakilishi wa wajumbe wa kigeni pia wamehudhuria sherehe hiyo pamoja na maelfu ya wageni walioalikwa. Lakini hapakuwa na rais yeyote aliyewakilisha nchini yake katika sherehe hiyo.

Patrice Talon kisha alitoa hotuba yake, akirejea masuala muhimu yatakayopewa kipaumbele katika muhula wake mmoja kipekee. Amerejelea mara kadhaa mageuzi ya kisiasa, kufufua uchumi na ujuzi. "Ninajikubalisha kuanza katika hatua hii, ninajiaminii," rais mpya amesma.

 

Kabla ya sherehe hiyo, Patrice Talon hatimaye alikutana na mtangulizi wake,Thomas Boni Yayi, katika Ikulu ya Rais mjini Cotonou.

Kulingana na taarifa zetu, Uamuzi huo ulichukuliwa Jumanne, Aprili 5 jioni. Karibu saa 2:45 usiku, rais anayemaliza muda wake alimpokea Patrice Talon katika Ikulu ya Marina. Wawili hao walipeana mikono, na kisha walifanya mazungumzo ya faragha kwa muda wa dakika ishirini katika Ikulu ya Marina.

Kisha, kama ishara, Patrice Talon alimshindikia Boni Yayi hadi kwa gari lake. Rais huyo wa zamani alijielekeza nyumbani kwake mjini Cotonou. Raia wa Benin kwa kweli wameshuhudia, picha walioku wakiisubiri kwa muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.