Pata taarifa kuu
Somalia

Mkutano unaolenga kutafuta amani nchini Somalia, waanza jijini Kampala

Mkutano wa kimataifa kuhusu usalama nchini Somalia na katika ukanda wa Afrika Mashariki unaendelea jijini Kampala, Uganda huku ukiwakutanisha wajumbe kutoka Afrika Mashariki na Kati na duniani kwa ujumla.Maudhui ya mkutano huo ni kutafuta namna ya kupata suluhu la kudumu nchini Somalia, taifa lililoshuhudia machafuko kwa muda mrefu sasa.

Wapiganaji wa Hisbul Islam katika mitaa ya Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.
Wapiganaji wa Hisbul Islam katika mitaa ya Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. Photo: Reuters
Matangazo ya kibiashara

Suala la kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabab, nalo limepewa nafasi kubwa katika mkutano huo.

Mkutano huo ni wa kumi na tisa tangu mzozo wa Somalia uanze kushughulikiwa kimataifa, na mwandishi wetu Tony Singoro wa jijini Kampala, amemhoji Balozi Augustine Mahiga, wa Mamlaka ya Maendeleo katika nchi za Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan, Uganda na Eritrea (IGAD) nchini Somalia, juu ya dhima ya mkutano huo.

Akifungua mkutano huo, Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewashauri marais wengine kuhakikisha wanaunganisha nguvu na kuhakikisha wanafikia muafaka, juu ya njia ya kuleta amani ya kudumu katika eneo hilo.

Na kwa upande wake Rais wa Somalia Sheikh Shariff Ahmed amesema kuwa mazungumzo baina ya serikali hiyo ya mpito na waasi huenda yakazaa matunda.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.