Pata taarifa kuu
CAF-MANE-SOKA

Tuzo za CAF: Sadio Mané achaguliwa mchezaji bora mwaka 2019

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mané amechaguliwa mchezaji bora wa mwaka 2019 kutoka barani Afrika. Sadio Mané alishiriki kinyang'anyiro hicho na wenzie wa Misri Mohamed Salah na Riyad Mahrez wa Algeria.

Sadio Mané akiwa na jezi ya Liverpool katika mchuano wa Ligi ya Mabingwa, Machi 13, 2019 dhidi ya Bayern.
Sadio Mané akiwa na jezi ya Liverpool katika mchuano wa Ligi ya Mabingwa, Machi 13, 2019 dhidi ya Bayern. GUENTER SCHIFFMANN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mané alichukua tuzo yake katika sherehe zilizofanyika huko Hurghada, nchini Misri.

Mane, mwenye umri wa miaka  27, alipata tuzo hiyo siku ya Jumanne usiku jijini Cairo nchini Misri, baaa ya kuisaidia klabu yake kunyakua taji la klabu bingwa barani Ulaya msimu wa mwaka 2018-19.

Baada ya tuzo hiyo, Mane alionesha furaha yake na kusema mchezo wa soka ni kazi yake anayoipenda sana.

" Nimefurahi sana kushinda tuzi hii.Mchezo wa soka ni kazi yangu," amesema Mane.

Hata hivyo, hafla hiyo haikuhudhuriwa na Salah na Mahrez ambao walikuwa wamepewa nafasi ya kushinda taji hilo.Wawili hao wamewahi kushinda taji hilo.

Mbali na Mane, kikosi bora barani Afrika kilitajwa:

Andre Onana (Ajax/Cameroon),

Achraf Hakimi (Borussia Dortmund/Morocco),

Kalidou Koulibaly (Napoli/Senegal),

Joel Matip (Liverpool/Cameroon),

Serge Aurier (Tottenham/Ivory Coast),

Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria),

Idrissa Gana Gueye (Paris St-Germain/Senegal),

Hakim Ziyech (Ajax/Morocco),

Mohamed Salah (Liverpool/Egypt),

Sadio Mane (Liverpool/Senegal),

Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal/Gabon).

Kwa upande wa akina dada, mchezaji kutoka Nigeria na anayechezea klabu ya Barcelona Asisat Oshoala alitajwa kuwa mchezaji bora.

Kocha Djamel Belmadi, aliyeisadia Algeria kunyakua taji la Afrika mwaka 2019 alitajwa kuwa kocha bora wa mwaka huku Diseree Ellis, akishinda tuzo ya kocha bora kwa upande wa wanawake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.