Pata taarifa kuu
WADA-URUSI-OLIMPIKI-TOKYO-JAPAN

Rais Putin akasirishwa na hatua ya WADA kuifungia Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin, amelaani hatua ya Shirika la dunia linalopambana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli au kuongeza nguvu mwilini kwa wanamichezo WADA, kwa kuifungia nchi yake kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya michezo kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Alexander Zemlianichenko/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya WADA, inamaanisha kuwa, Urusi haitashiriki katika michezo ya Olimpiki mwaka 2020, itakayofanyika jijini Tokyo nchini Japan lakini pia kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Hatua hii imekuja, baada ya maafisa wa WADA kukutana jijini Lausanne, nchini Uswizi baada ya kuishtumu serikali ya Urusi kwa kufanya udanganyifu kuhusu matokeo ya vipimo vya wanamichezo waliofanyiwa ucbunguzi mapema mwaka huu.

Adhabu hii pia inawazuia viongozi wa serikali kutoshiriki katika matukio makubwa ya michezo, lakini pia Urusi haitaweza kuwa mwenyeji wa ma mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Rais wa WADA, Craig Reedie amesema kuwa Urusi ilipewa fursa ya kipekee ya kujisafisha ili kurejea tena katika ulimwengu wa michezo, lakini imeendelea kukanusha kuwasaidia wanamichezo wake hasa wanariadha kutumia dawa za kuwaongezea nguvu mwilini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.