Pata taarifa kuu
RWANDA-PSG-BIASHARA-SOKA

Rwanda mdhamini mpya wa Paris Saint-Germain kwa miaka mitatu

Mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa PSG (Paris Saint Germain wametangaza kwamba wamefikia makubaliano ya ushirikiano wa miaka tatu na serikali ya Kigali bila kutaja kiwango cha fedha.

Wachezaji wa PSG, pamoja na Neymar kutoka Brazil, watavaa jezi zenye nembo ya "Tembelea Rwanda" msimu ujao.
Wachezaji wa PSG, pamoja na Neymar kutoka Brazil, watavaa jezi zenye nembo ya "Tembelea Rwanda" msimu ujao. © FRANCK FIFE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Mei 2018, Rwanda ilisaini makubaliano ya aina hii na Arsenal, yaliyokadiriwa kufikia thamani ya karibu dola milioni 40.

Ushirikiano kati ya PSG na Rwanda unalenga kukuza utalii na biashara, hususan bidhaa za Rwanda.

Kuanzia msimu ujao, uwanja wa mpira wa Parc des Princes, unaomilikiwa na PSG utakuwa na mabango yenye rangi ya nembo ya 'Visit Rwanda', Tembelea Rwanda, maneneo yanayolenga kuvutia watalii zaidi nchini humo.

"Bango lenye maneno 'Tembelea Rwanda' litaonyeshwa katika uwanja wa Parc des Princes, kwenye fulana za timu ya wanawake ya Paris Saint-Germain pamoja na nyuma ya nguo zao za mazoezi", tangazo hilo limesema.

Bodi ya mamlaka ya maendeleo ya Rwanda, imetangaza kwamba chini ya makubaliano hayo, majani chai na kahawa kutoka Rwanda,vitauzwa katika uwanja wa michezo wa Paris Saint Germain.

Kulingana na Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Rwanda (ADB) Bi Clare Akamanzi mapatano yaliyosainiwa kati ya serikali ya Rwanda na club ya Ufaransa ya Paris Saint Germain ni mapana yakihusu sekta mbali mbali.

Na kila mwaka tutakuwa na kampeni ya wiki nzima inayofahamika kama Rwanda week mjini Paris ni kama wiki ya maonyesho ya bidhaa na utamaduni wa Rwanda mjini Paris'' amesema Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.