rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CECAFA Kenya Djibouti Ethiopia Uganda Tanzania

Imechapishwa • Imehaririwa

Michuano ya CECAFA kwa wanawake yaendelea, Kenya yasaka ushindi wa pili

media
Timu ya taifa ya soka ya wanawake HarambeeĀ Starlets Harambee Starlets/Twitter.com

Kenya inatafuta ushindi wake wa pili katika michuano ya soka kwa wanawake kuwania taji la Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inayoendelea jijini Dar es salaam nchini Tanzania.


Harambee Starlets itamenyana na Djibouti, huku Ethiopia ikimenyana na Uganda.

Siku ya Jumatatu, Sudan Kusini iliishinda Zanzibar mabao 5-0, huku Tanzania ikiwaangusha Burundi mabao 4-0.

Sudan Kusini nayo itamenyana na Burundi siku ya Jumatano kutafuta ushindi wake wa pili, huku Zanzibar ikimenyana na Tanzania bara.

Uganda na Kenya zote zina alama tatu, huku Tanzania ikiongoza kundi la B kwa alama 6 baada ya kushinda mechi zake mbili.

Burundi na Sudan Kusini baada ya kupata ushndi wa kwanza, zina alama tatu.

Matokeo yaliyopita:-

Burundi 5-0 Zanzibar

Kenya 0-2 Ethiopia

Sudan Kusini 5-0 Djibouti

Tanzania 9-0 Sudan Kusini

Uganda 13-0 Djibouti

Tanzania 4-0 Burundi