rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Kenya Zambia

Imechapishwa • Imehaririwa

Michuano ya kufuzu michezo ya fainali mwaka 2020 yaingia hatua ya mwisho

media
Harambee Starlets ya Kenya KPL

Mzunguko wa nne kufuzu katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika nchini Japan mwaka 2020 kwa upande wa wanawake barani Afrika, inachezwa mwishoni mwa wiki hii.


Mataifa yanayowania nafasi hiyo ni pamoja na Kenya, Zambia, Cameroon na Ivory Coast.

Harambee Starlets ya Kenya itachuana na The She-polopolo ya Zambia katika mchuano wa mzunguko wa kwanza, mechi itakayochezwa Ijumaa jioni katika uwanja wa Kimataifa wa soka wa Kasarani jijini, Nairobi.

Siku ya Jumamosi, Ivory Coast itamenyana na Cameroon katika uwanja wa Treichville, jijini Abidjan.

Mechi hizi zinachezwa nyumbani na ugenini na mshindi atafuzu katika hatua ya mwisho, mechi zitakazopigwa nyumbani na ugenini mwezi Januari mwaka 2020.

Timu itakayoshinda ndiyo itakayofuzu lakini, ikayoshindwa itachezwa na mwakilishi aliyemaliza katika nafasi ya pili kutoka bara la Amerika Kusini CONMEBOL.