rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Tanzania CHAN

Imechapishwa • Imehaririwa

Kocha Migne kwa FKF: Nifuteni kazi mkitaka

media
Kocha wa Harambee Stars Sebastien Migne FKF

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Mfaransa Sebastian Migne amesema, rais wa Shirikisho la soka nchini humo Nick Mwendwa anaweza kumfuta kazi iwapo anataka kufanya hivyo.


Migne ametoa kauli hii baada ya Kenya kuondolewa na Tanzania katika michuano ya kufuzu kucheza fainali ya CHAN Jumapili iliyopita, baada ya kufungwa mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti, jijini Nairobi.

Mechi hiyo ilifikia katika hatua hiyo, baada ya timu zote kutofungana katika muda wa kawaida, katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani.

“Iwapo Shirikisho linataka kunifuta kazi, liendelee kufanya hivyo, lakini nina mashaka iwapo linaweza kunilipa, iwapo litavunja mkataba wangu,” alisema.

“Iwapo wanapata wakati mgumu kulipa mshahara wangu, je wataweza kutekeleza mkataba wangu,” aliongeza.

Uongozi wa soka nchini Kenya, haujajitokeza kuzungumzia hatima ya kocha huyo kuendelea kuifunza Harambee Stars.

Migne alisaini mkataba wa miaka mitatu mwaka 2018, kuifunza Harambee Stars na baada ya AFCON mwaka 2019, ana kazi ya kuisaidia nchi hiyo kufuzu katika michuano ya 2021 na ile ya kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar.