rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Timu ya Taifa ya DRC Kenya

Imechapishwa • Imehaririwa

DRC yaishinda kenya na kunyakua taji la kikapu Afrika

media
Kenya iliishinda Morocco katika mchezo wa nusu fainali CGTN Africa

Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetwaa ubingwa wa mchezo wa kikapu barani Afrika.


Ubingwa wa DRC umekuja baada ya kuishinda Kenya kwa vikapu 82 kwa 61 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Bamako nchini Mali.

Kongo iliongoza kwa vikapu 11 kabla ya Kenya kujibu mapigo kwa vikapu 19 kwa 7 katika mzunguko wa pili.

Mzunguko wa tatu DRC iliongoza kwa vikapu 29 kwa 10 kabla ya DRC kuongoza mzunguko wa nne kwa vikapu 17 kwa 14.

Maxi Shamba wa DRC alifunga vikapu 20 na kufanikisha Rebound saba.

Tylor Ongwae wa Kenya alifunga vikapu 21 katika mchezo huo.

Angola ilimaliza ya tatu katika mashindano hayo kwa kuishinda Morocco kwa vikapu 88 kwa 71.

Mashindano hayo yalishirikisha timu 12 huku Afrika Mashariki ikiwakilishwa na Kenya pekee.