Pata taarifa kuu
CHAN 2020-AFRIKA-SOKA-MASHARIKI-KATI

Mataifa ya Afrika mashariki yapambana kufuzu CHAN 2020

Michuano ya soka mzunguko wa kwanza, kuwania fainali ya bara Afrika kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani mwaka 2020 nchini Cameroon, itachezwa mwishoni mwa wiki.

Timu ya taifa ya soka ya Uganda, inayowajumuisha wachezaji wanaocheza soka nyumbani
Timu ya taifa ya soka ya Uganda, inayowajumuisha wachezaji wanaocheza soka nyumbani www.fufa.co.ug
Matangazo ya kibiashara

Mataifa 16 yatashiriki katika michuano hiyo na yatafuzu kutoka kanda zote za mchezo wa soka barani Afrika.

Eneo la Afrika Mashariki na Kati, itatoa mataifa mawili yatakayofuzu katika michuano hiyo, na mechi hizi zinachezwa nyumbani na ugenini katika mzunguko wa kwanza na wa pili.

Rwanda na Sudan tayari zimefuzu katika mzunguko wa pili na zinasubiri wapinzani wao mwezi Septemba.

Siku ya Ijumaa, Djibouti watamenyana na Ethiopia, huku Burundi wakiwakaribisha Sudan Kusini na Somalia dhidi ya Uganda siku ya Jumamosi.

Siku ya Jumapili, Tanzania itamenyana na Kenya jijini Dar es salaam kabla ya mechi ya marudiano siku ya mapema mwezi Agosti jijini Nairobi.

Fainali ya kwanza ya CHAN iliandaliwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast na DRC kuwa mabingwa wa kwanza.

Morocco walikuwa wenyeji walikuwa wa mwisho kuandaa michuano hii mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.