rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Senegal Benin AFCON 2019

Imechapishwa • Imehaririwa

AFCON 2019: Senegal yatinga nusu fainali

media
Senegal wakisherehekea bao la Idrissa Gana Gueye dhidi ya Benin katika robo fainali za AFCON 2019. RFI/Pierre René-Worms

Senegal itacheza imeingia katika nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu 2006, baada ya kuiadhibu Benin Julai 10 jijini Cairo, nchini Misri 1-0.


Furaha ilio je kwa "Simba" kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu. Hata hivyo Senegal imeapa kutwa Kombe la Afcon mwaka huu.

Ni kizazi kipya ambacho kimefanya Senegal kupiga hatua kubwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Tunataka kuwea historia kwa nchi yetu. Henri Saivet, kiungo wa kati wa Simba, amesema, huku akiwa na imani ya kuendelea hadi mchuano wa mwisho wa fainali. Hata hivyo amepongeza timu yake na ushindi walioupata licha ya kuwa haikuwa rahisi dhidi ya timu ya taifa ya Benin.

"Tangu kuanza kwa michuano hii ya AFCON 2019, hakuna mechi ambayo ni rahisi, amesema Henri Saivet.

“Tumekutana na timu ambao haikuwa rahisi kuifunga. Katika hatua ya makundi, hatukupoteza dhidi ya Cameroon na Ghana. Kisha tuliweza kuwaondoa Morocco katika mzunguko wa 16. Katika mchuano wetu na Benin, tulijua kwamba itachukua muda kuwaangsha. Lakini hatukuwa na hofu. Tulijua nini cha kufanya. Bodi ya usimamizi walifanya kazi kubwa ili tuweze kuwaangusha Benin pamoja na kuwa haikuwa rahisi, " ameongeza Henri Saivet, kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Senegal.