rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Nigeria Cameroon

Imechapishwa • Imehaririwa

Michuano ya kombe la dunia kwa wanawake yaingia hatua ya robo fainali

media
Wachezaji wakipongezana baada ya mechi muhimu www.fifa.com

Michuano ya robo fainali kuwania taji la kombe la dunia katika mchezo wa soka kwa upande wa wanawake inaendelea siku ya Alhamisi, nchini Ufaransa.


Mechi ya kwanza itakuwa kati ya Norway na Uingereza, katika uwanja wa Oceane, Le Havre.

Siku ya Ijumaa, Ufaransa itamenyana na Marekani.

Italia na Uholanzi zitachuana siku ya Jumamosi, huku Ujerumani na Sweden zikipambana.

Wawakilishi wa Afrika, Cameroon na Nigeria waliondolewa katika hatua ya 16 bora.

Ujerumani iliishinda Nigeria mabao 3-0 huku Uingereza nayo ikiishinda Cameroon mabao 3-0.

Wawakilishi wengine wa Afrika waliondolewa katika michuano hii ni Afrika Kusini.