rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Burundi Kenya Tanzania AFCON 2019

Imechapishwa • Imehaririwa

Nchi tatu za Afrika mashariki zaanza vibaya AFCON

media
Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba. RFI-KISWAHILI

Timu za taifa za mchezo wa soka za Kenya na Tanzania, zimeanza vibaya michuano inayoendelea kuwania taji la bara Afrika nchini Misri, huku baadhi ya mataifa yakiendelea vizuri.


Taifa Stars ilikuwa timu ya kwanza kufungwa na Senegal mabao 2-0 na baadaye Harambee Stars kupoteza pia kwa mabao 2-0 dhidi ya Algeria, katika mechi za kundi C.

Wawakilishi hao wa Afrika Mashariki, walionekana kuelemewa katika mechi zao, na watanarajiwa kumenyana baadaye wiki hii.

Burundi na DRC ni timu nyingine zinazowakilisha ukanda wa Afrika, zilizoanza vibaya, lakini Uganda ilianza kwa matumaini baada ya kuishinda DRC mabao 2-0.