rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Guinea

Imechapishwa • Imehaririwa

Horoya yamsajili mchezaji aliyeachwa na Azam

media
Mchezaji Enock Atta Agyei amesajiliwa na Horoya ya Guinea baada ya kuachwa na Azam FC Twiiter/Enock Atta

Timu ya Horoya ya Guyinea imemsajili mchezaji Enock Atta Agyei siku chache baada ya kutangazwa kuachwa na klabu ya Azam FC ya Tanzania.


Atta anakuwa mchezaji wa tatu kutoka ligi ya Tanzania kusajiliwa na klabu hiyo baada ya Tafadzwa Kutinyu na Heritier Makambo.

Ripoti kutoka nchini Guinea zilizochapishwa na gazeti la michezo la Mwanaspoti nchini Tanzania zinasema mchezaji huyo ametia kandarasi ya miaka mitano.

Nyota wengine walioachwa na Azam ni Ramadhan Singano, Obrey Chirwa, Steven Kingue, Danny Lwanga, Hassan Mwasapili na Joseph kimwaga.