rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Misri CAF

Imechapishwa • Imehaririwa

Harambee Stars yatua Misri na matumaini kibao

media
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars wakiwa kambini nchini Ufaransa FKF

Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars imewasili nchini Misri kushiriki fainali za mataifa ya Afrika huku ikiwa na matumaini lukuki ya kufanya vyema katika fainali hizo.


KKenya inarejea katika mashindano hayo baada ya miaka 15 tangu iliposhiriki fainali za mwaka 2004 zilizofanyika nchini Tunisia ambapo wenyeji Tunisia waliibuka washindi kwa kuifunga Morocco kwa mabao 2-1.

Ikiwa kambini nchini Ufaransa Kenya ilicheza mechi mbili za kujipima nguvu na Madagascar na DR Congo.

Kikosi cha Kenya kinachonolewa na mfaransa Sebastien Migne kimefikia katika hoteli moja iliyopo katikati ya jiji la Cairo.

Kenya imepangwa Kundi C la michuano hiyo ikiwa pamoja na Tanzania, Senegal na Algeria na mchezo wake wa kwanza itachuana na Algeria Juni 23 kisha kuchuana na Tanzania Juni 27 na mechi ya mwisho ya hatua ya makundi itakuwa dhidi ya Senegal Julai 1.