Pata taarifa kuu
FRENCH OPEN

French Open: Petra Kvitova ajitoa, Federer arejea kwa kishindo

Bingwa mara mbili wa michuano ya tenesi ya Wimbledon, Petra Kvitova amejiondoa katika raundi ya kwanza ya michuano ya French Open kutokana na majeraha ya mkono.

Petra Kvitova akiwa katika moja ya mechi zake.
Petra Kvitova akiwa katika moja ya mechi zake. Reuters/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Kvitova raia wa Jamhuri ya Czech na anayeshikilia nafasi ya 6 kwa ubora wa mchezo huo duniani, alikuwa acheze na Sorana Cirstea raia wa Romania.

Mchezaji huyo pia ametangaza kuwa hatashiriki michuano ya Italian Open inayitarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi huu mjini Rome ambapo alitarajiwa kucheza na Maria Sakkari raia wa Ugiriki.

“Nimekuwa na maumivu kwenye mkono wangu kwa wiki kadhaa sasa na usiku wa jana vipimo vya MRI vimeonesha nna jeraha,” alisema Kvitova wakati akitangaza kujiondoa.

Katika mechi za hapo jana kwa upande wa wanaume, mchezaji Roger Federer alifanikiwa kutinga mzunguko wa pili baada ya kumfunga Lorenzo Sonegop kwa seti tatu mfululizo.

Federer ambaye ana mataji 20 kibindoni, alishinda kwa matokeo ya 6-2, 6-4 na 6-4.

Matokeo mengine ni kuwa Stefanos Tsitsipas alimfunga Maximilian Marterer kwa seti 6-2, 6-2, 7-6 (7/4) huku Hugo Dellien akimfunga Prajnesh Gunneswaran kwa seti 6-1, 6-3, 6-1.

Kei Nishikori wa Japan yeye akamfunga Quentin Halys wa Ufaransa kwa seti 6-2, 6-3, 6-4, huku Alexei Popyrin akimfunga Ugo Humbert kwa seti 3-6, 6-3, 7-6 (12/10), 6-3.

Kwa upande wa wanawake mchezaji Sloane Stephens wa Marekani alimfunga Misaki Doi wa Japan kwa seti 6-3, 7-6 (7/3), huku Sara Sorribes akimfunga Alison Van Uytvanck kwa seti 6-1, 5-7, 6-2.

Garbine Muguruza wa Hispania akamfunga Taylor Townsend wa Marekani kwa seti 5-7, 6-2, 6-2, huku Elina Svitolina wa Ukraine akimfunga Venus Williams kwa seti 6-3, 6-3.

Michuano hiyo inaendelea tena Jumatatu hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.