rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon Guinea CAF

Imechapishwa • Imehaririwa

Cameroon yaizamisha Guinea na kutwaa taji lake la pili

media
Les Lions Indomptables, ilishinda mechi hiyo dhidi ya Guinea baada ya kutoka sare ya 0-0 kwqa mikwaju (5-3). Fecafoot-Officiel/twitter.com

Cameroon imeshinda taji lake la pili katika mashindano ya vijana wasiozidi miaka 17, baada ya kuilaza Guinea katika mchuano wa fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania.


Les Lions Indomptables, ilishinda mechi hiyo baada ya kupata mikwaju ya penalti 5-3, baada ya mchuano huo kumalizika kwa kutofungana.

Mara ya kwanza Cameroon kushinda taji hilo, ilikuwa mwaka 2003, wakati huo, mashindano haya yalifanyika nchini Swaziland.

Pamoja na kushinda taji hili, Cameroon itaongoza wawakilishi wengine wa Afrika, Guinea, Angola na Nigeria kwenda kutafuta ubingwa wa dunia nchini Brazil mwezi Oktoba.

Mataifa mengine ambayo yamewahi kushinda taji hili la vijana ni pamoja na Ghana mara mbili mwaka 1995, 1999.

Nigeria pia imeshinda mara mbili, sawa na Gambia pamoja na Mali iliyoshinda mwaka 2015 na 2017.

 

Burkina Faso, Cote d'Ivoire na Misri wameshinda mara moja.