rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CAF Afrika Kombe la Shirikisho Afrika Tanzania

Imechapishwa • Imehaririwa

CAF kutumia waamuzi wawili zaidi michuano ya nusu fainali kuwania taji la vijana

media
Michuano ya vijana barani Afrika www.cafonline.com

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, kwa mara ya kwanza, litawatumia waamuzi wa ziada katika mechi muhimu za hatua ya nusu fainali, kuwania taji la bara Afrika baina ya vijana wasiozidi miaka 17, inayoendelea nchini Tanzania.


Wasaidi wa waamuzi hao watakuwa wawili na kila mmoja, atakuwa nyuma ya goli, ili kuhakikisha kuwa sheria za mchezo wa soka zinaheshimiwa ili kuzuia mvutano wowote hasa kuhusu ufungaji wa goli.

Mechi ya kwanza ya nusu fainali itakuwa ni kati ya Nigeria na Guinea, kuanzia saa 10  jioni  saa za Afrika Mashariki, katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Nigeria ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kumaliza ya kwanza katika kundi A kwa alama 7 huku Guinea ikimaliza kundi la B kwa alama 6.

Mechi ya pili ya nusu fainali, itawakutanisha Cameroon na Angola kuanzia saa moja na nusu  usiku, saa za Afrika Mashariki.

Washindi watakutana katika fainali, itakayochezwa siku ya Jumapili.

Mbali na michuano hiyo ya nusu fainali, Nigeria, Guinea, Cameroon na Angola zote zimefuzu katika fainali ya kombe la dunia baina ya vijana, itakayofanyika nchini Brazil mwezi Oktoba.

Wenyeji Tanzania na Uganda kutoka eneo la Afrika Mashariki, waliondolewa mapema katika mashindano haya makubwa kwa vijana barani Afrika.