rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania CAF Nigeria Guinea Cameroon Angola

Imechapishwa • Imehaririwa

Afrika U-17: Nigeria, Guinea, Cameroon na Angola kupimana nguvu

media
Wakati wa mechi kati ya Nigeria na Cameroon katika michuano ya Kombe la Afcon kwa vijana wasiozidi miaka 17 mnamo mwaka 2011. CAF

Mechi za nusu fainali kuwania taji la bara Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka kumi na saba (U 17), itachezwa leo Jumatano Aprili 24 nchini Tanzania.


Mechi zote zitachezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Nigeria watakuwa wa kwanza, kumenyana na Guinea kuanzia saa 10 jioni lakini baadaye Cameroon watamenyana na Angola kuanzia saa moja na nusu.

Fainali itachezwa siku ya Jumapili.

Mataifa haya manne, Nigeria, Guinea, Cameroon na Angola, zote zimefuzu katika fainali ya kombe la dunia kwa vijana utakayofanyika mwezi Oktoba nchini Brazili.