rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

AFCON Tanzania Cameroon

Imechapishwa • Imehaririwa

Cameroon yafuzu nusu fainali michuano ya vijana barani Afrika

media
Wachezaji wa Cameroon wakishangilia baada ya kuifunga Morocco 2-1 katika mechi muhimu ya kundi B April 18 2019 www.cafonline.com

Cameroon imefuzu katika hatua ya nusu fainali, ya michuano ya bara Afrika kwa vijana wasiozidi miaka 17 inayoendelea nchini Tanzania.


Indomitable Lions, walifika katika hatua hiyo baada ya kushinda mechi yake ya pili katika michuano ya kundi B. kwa kuifunga Morocco mabao 2-1 siku ya Alhamisi katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Chamazi.

Guinea nayo ilipata ushindi wake wa kwanza, baada ya kusihinda Senegal mabao 2-1 na ni ya pili katika kundi hilo kwa alama tatu.

Michuano hii itarejelewa kesho kutamatisha kundi la A, Tanzania watacheza na Angola huku Nigeria ikimaliza kazi na Uganda.

Nigeria, Angola na Uganda zina nafasi kubwa ya kufuzu katika nusu fainali.

Mataifa manne yatakayofika katika hatua ya nusu fainali, yatafuzu katika michuano ya kombe la dunia baadaye mwaka huu nchini Brazil.