rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon Guinea

Imechapishwa • Imehaririwa

Cameron waibwaga Guinea kwa 2-0

media
Lions indomptables watamba dhidi ya Guinea, kwenye uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam. RFI/Pierre René-Worms

Cameroon, mabingwa wa mwaka 2003 katika taji la soka barani Afrika kwa vijana wasiozidi miaka 17, wameanza vema mashindano yanayoendelea nchini Tanzania.


Lions Indomptables waliifunga Guinea mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Morocco na Senegal, nazo zilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya pili ya kundi B.

Cameroon inaongoza kundi la B kwa alama tatu huku Morocco, Senegal na Guinea zikiwa na alama moja.

Michuano hii itarejelewa siku ya Jumatano.

Nigeria inayoongoza kundi la A kwa alama tatu, itamenyana na Uganda baada ya kuwashinda wenyeji Tanzania mabao 5-4.

Tanzania nayo itachuana na Angola, ambayo mechi ya kwanza iliishinda Uganda bao 1-0.