Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA

Klabu nne zafuzu katika taji la Shirikisho Afrika

Klabu za CS Sfaxien ya Tunisia, RS Berkane ya Morocco na Zamalek ya Misri zimefuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.

Mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa wawakilishi wa Kenya, Gor Mahia ambao katka mechi ya marudiano walifungwa mabao 5-1.
Mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa wawakilishi wa Kenya, Gor Mahia ambao katka mechi ya marudiano walifungwa mabao 5-1. gormahiafc.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya michuano ya mzunguko wa pili wa robo fainali mwishoni mwa wiki iliyopita

CS Sfaxien iliishinda Nkana ya Zambia kwa mabao 2-0 katika emchi yake ya pili, lakini Zamalek iliishinda Hassania Agadir bao 1-0.

Hata hivyo, mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa wawakilishi wa Kenya, Gor Mahia ambao katka mechi ya marudiano walifungwa mabao 5-1.

Hii imechangiwa na wachezaji wa klabu hii kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuwasili nchini Morocco kwa kuchelewa lakini pia baadhi ya wachezaji walionekana wakiwa wamelala katika uwanja wa ndege wa Doha, suala ambalo limezua maswali mengi.

Mechi kati ya Al Hilal ya Sudan na Etoile du Sahel haikuchezwa kwa sabbau za kiusalama nchini Sudan.

CS Sfaxien itamenyana na RS Berkane katika mechi ya nusu fainali, huku Zamalek ikisubiri mechi ya mwisho kati ya Al-Hilal na Etoile du Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.